Michezo

Arsene Wenger awatupia lawama mashabiki adai wamekosa umoja

Mara baada ya meneja wa Arsenal, Arsene Wenger siku ya Ijumaa kutangaza kuondoka ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu, Jumapili hii amewatupia lawama mashabiki kwakukosa umoja hali inayopelekea kuaribu taswira ya timu hiyo.

Kwa mara ya kwanza jana siku ya Jumapili, Wenger ameeleza sababu ya maamuzi yake ya kuachia ngazi ambapo amesema kuwa hakuchoka kuifundisha timu hiyo bali aliamua kufanya hivyo baada ya kuona baadhi ya mashabiki wakiandamana wakimuhitaji aondoke jambo ambalo limekuwa likimuumiza na kuvuruga taswira ya klabu.

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 68 hapo jana aliamua kuweka wazi sababu zilizomfanya kumaliza ukomo wa utawala wake wa miaka 22 ndani ya klabu ya Arsenal.

Sikuchoka kuifundisha Arsenal, wenga ameyasema hayo mara baada ya kupata ushindi wa jumla ya mabao 4 – 1 dhidi ya West Ham.

Sikuchoka kuifundisha Arsenal, binafsi ninaamini hii klabu inaheshima dunia nzima, ni zaidi hata ya Uingereza. Mashabiki wetu hawana umoja na hivyo kujenga taswira mbaya kwa klabu jambo ambalo linaniuma, taswira hii tunayo ijengea timu yetu siyo kitu ambacho mimi nakipenda.

Sifanyi hivi kwa kutengeneza vichwa vya habari vya kijinga, nahitaji kile ninachokifikiria kwenye klabu yangu kifanikiwe na hicho ndiyo kitu muhimu pekee  kwangu.

Nimesafiri sana na klabu hii na kujionea namna inavyoheshimika duniani, tunaangushwa kwa namna tunavyocheza, kwa namna ya tabia zetu zilivyo kwa sasa na vile tunavyo wafanya watu watuchukulie hivyo nahitaji kuondoka na kuiacha taswira ya timu ikiwa kwenye muonekano mzuri. Ijapokuwa kuna fedha nyingi kwenye mchezo zaidi hata ya matokeo ya uwanjani.

Wenger amejiunga na Arsenal mwaka 1996  akiwa ni meneja wa pili kutoka nje ya Uingereza au Ireland kupata nafasi ya kuzinoa timu za nchi hiyo na kuisaidia kwa kiwango kikubwa mabadiliko ya soka Epl.

Akifanikiwa kutwaa taji la ligi akiwa na Arsenal mwaka 1998, 2002 na 2004 bila kufungwa ‘Invincibles’ msimu mzima huku ikifanikiwa kuvutia mashabiki.

Wenger amesema kuwa mchezo ni zaidi ya kushinda au kufungwa kiasi kwamba anadhani kubwa kwake ni kuhakikisha anatanua wigo kwa timu hiyo kwa watoto wanaopenda soka Afrika, China,  America. na lengo lake kubwa ni kuzalisha vipaji kwa vijana wadogo.

Mfaransa huyo amesema kuwa kuna Arsene Wenger mmoja tu uwanja wa Emirates. Ninajiskia furaha pale mashabiki wanapokuwa na furaha.

Najaribu kuvutia miundombinu ya klabu na maendeleo ya mchezaji mmoja mmoja na kuwekeza katika aina ya uchezaji wetu. Ninaamini nitaiyacha timu hii ikiwa na mipango imara na hiyo ilikuwa lengo langu lakini pia kumuachia nafasi mrithi wangu atakae kuja kuchukua nafasi hii na pengine kufanya vema zaidi yangu mimi kwa miaka 20 ijayo, hilo ndilo tarajio langu.

Nafasi kubwa ya Arsenal iliyopo kwa sasa ni michuano ya Europa League hatua ya nusu fainali dhidi ya Atletico Madrid siku ya Alhamisi. Kwa kuwa sasa Arsenal ipo nje ya ‘top four’ kwenye msimamo wa ligi ya Uingereza ikitwaa ubingwa huo itapata nmafasi ya kushiriki Champions League.

Nimetumia miaka yangu 22 ndani ya klabu na niliipatia miaka yenye mafanikio, nilikuja hapa nikiwa na miaka 46 na nilifanya kazi kwa siku saba bila hata kupumzika ni siyo sita bali siku saba kwa wiki nzima. Najua nitapitia wakati mgumu kwenye maisha yangu baada ya kuachana na timu hii lakini nawashukuru sana na nasema kwaherini.

Wenger mpaka sasa hajatangaza kama atakwenda kujiunga na klabu gani licha ya kuwa huwenda asifundishe Uingereza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents