Michezo

Arsene Wenger bado yupo yupo sana aipiga AC Milan kwao (+picha)

Kikosi cha meneja wa Arsenal, Arsene Wenger hapo jana siku ya Alhamisi kilifanikiwa kuchomoza na ushindi mnono wa mabao 2 – 0 ugenini dhidi ya AC Milan hatua ya 16 bora ya michuano ya Europa League.

Waliyo funga magoli hayo ni Henrikh Mkhitaryan dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza na Aaron Ramsey akikamilisha idadi hiyo ya mabao kwa kufunga la pili dakika ya 45 kabla ya kwenda mapumziko.

Kwa matokeo hayo ya mabao 2 – 0 sasa yanaifanya the Gunners kuwa na nafasi kubwa ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo endapo wataweza kulinda matokeo yao siku ya Alhamisi katika dimba la Emirates.

Baada ya matokeo hayo meneja wa klabu ya Arsenal, Mzee Wenger amesema kuwa yote kinachotakiwa ni ushindi.

Kinachotakiwa na kilicho muhimu kwetu ni ushindi tu, lakini siyo utimamu. Ni lazima tukamilishe kazi nyumbani, ninafuraha kuona juhudi zilizofanywa na wachezaji wangu.

Hatupo katika nafasi ya kupoteza lakini hatupaswi kujiamini sana, tutapaswa kuendelea kuwa kimya hadi mwisho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents