Michezo

Arsene Wenger kutua Bayern Munich, mwenyewe akiri hilo

Arsene Wenger anatarajia kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Bayern Munich juu ya kuangalia uwezekano wa kuwa kocha wa miamba hiyo ya soka ya Bundesliga baada ya kuachishwa kazi kwa aliyekuwa mwalimu wa timu hiyo Niko Kovac.

Image result for Arsene Wenger to Bayern Munich

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Bayern, Karl-Heinz Rummenigge mapema alisema kuwa hana mpango na Wenger, ambaye amekuwa nje ya ajira tangu alivyoondoka Arsenal mwaka 2018.

Lakini kocha huyo wa zamani wa Gunners mwenye umri wa miaka 70, amekiri kuwepo na hilo huku kuiyambia Bein Sports kwamba kwa pamoja na Bayern wameamua kulizungumzia hilo wiki ijayo “Kwa pamoja tumeamua kulizungumzia hilo wiki ijayo, kwasababu hivi sasa nipo Doha, Qatar na nitakuwa huku hadi siku ya Jumapili, na hii ndiyo stori ya kweli.” amesema Wenger.

“Mchana wa siku ya Jumatano, Rummenigge alinipigia. Lakini nisingeliweza kumjibu na kwa heshima nilikuja kumpigia baadaye.”

“Alikuwa kwenye gari lake akienda kwenye mchezo dhidi ya Olympiacos. Tuliongea kwa takribani dakika nne ama tano na kuniambia kwamba wamemsajili Hans-Dieter Flick kuwa kocha ambaye atasimamia mechi mbili zijazo.”

“Rummenigge aliniuliza kama nitavitiwa na Bayern kwasababu wanatafuta kocha, nikamwambia sikuwahi kufikiria kuhusu hilo hivyo naomba muda wa kufiria.”

Mfaransa huyo, Wenger ameshinda mataji matatu ya Premier na saba ya FA Cups kwenye kipindi chake cha miaka 22 ambacho ameitumikia Arsenal.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents