Michezo

Arturo Vidal afukuzwa na kocha wa timu ya taifa ya Chile kwa ulevi

Mchezaji wa timu ya taifa ya Chile na klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani, Arturo Vidal amefukuzwa na kocha wake, Jorge Sampaoli.

Vidali

Timu ya taifa ya Chile ipo kwenye maandalizi ya kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Paraguay. Wachezaji wote wapo kambini na wanaendelea na mazoezi lakini Vidal aliripoti kwenye kambi ya timu ya hiyo Jumanne mchana akiwa amelewa.

Kocha wake hakupendezwa na kitendo hicho na alimrudisha kwa kumwambia arudi Ujerumani hadi pale atakapokuwa tayari.

Kocha huyo pia alimpa onyo kali na amempa nafasi ya mwisho.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents