Habari

`ARVS zitoke kwenye viwanda halali`

Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na vijana mabalozi wa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (TAYOPA), limeiomba serikali kuhakikisha kuwa Dawa za Kurefusha Maisha (ARVs), zinazoingizwa nchini zinatoka katika viwanda vinavyofahamika.

Na Mwajabu Mleche

 
Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na vijana mabalozi wa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (TAYOPA), limeiomba serikali kuhakikisha kuwa Dawa za Kurefusha Maisha (ARVs), zinazoingizwa nchini zinatoka katika viwanda vinavyofahamika.

 

Hayo yamesemwa na Katibu wa Mabalozi hao, Bi. Anita Amir, wakati wa semina ya kujadili Haki za Wanawake na Ukimwi, iliyoandaliwa na taasisi ya Action Aids.

 

Alisema waathirika wengi wa ugonjwa wa Ukimwi, wameathiriwa na dawa ambazo zinatengenezwa na baadhi ya viwanda ambazo hazikidhi viwango vya ubora.

 

`Serikali iangalie sana madawa wanayoagiza kutoka nchi za nje, kwani waathirika wengi hupatwa na matatizo ya kuvimba mwili,` alisema.

 

Bi. Anifa alisema madhara yanayowakuta waathirika hao ni kuvimba miguu, matiti, matatizo ya msukumo wa damu na kubonyea uso.

 

Alisema uingizwaji wa dawa hizo unaashiria kuwa afya za waathirika, hazipewi kipaumbele hivyo huhatarisha maisha ya watumiaji.

 

Kuhusu unyanyapa, Bi. Amir alisema wanawake wanaowahudumia wagonjwa wa Ukimwi, hunyanyapariwa na kuambiwa kuwa nao wameathirika na ugonjwa huo.

 

`Wanawake wengi wanaojitolea kuwahudumia wagonjwa wanaoishi na virusi vya Ukimwi, hutengwa na watu hata na madaktari wanaowapa huduma hospitalini,` alisema.

 

Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents