Michezo

Asamoah Gyan kujiunga na klabu ya Reading ya Uingereza

Nahodha wa kikosi cha soka nchini Ghana Asamoah Gyan anatarajiwa kujiunga na klabu ya Reading kwa mkopo kutoka timu ya China Shanghai SIPG.

Asamoah Gyan in action for Ghana

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Sunderland anafanyiwa vipimo vya afya na klabu hiyo ya daraja la kwanza.

Gyan aliifungia mabao 30 Sunderland alipoichezea timu hiyo kwa misimu miwili,kutoka mwaka 2010 kabla ya kuelekea Al-Ain ya Umoja wa Milki za kiarabu UAE.

Alijiunga na Shanghai 2015 wakati huo na alikuwa miongoni mwa mchezaji wanaolipwa zaidi duniani.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents