Burudani

Asante Navy Kenzo kwa kuja kuiondoa ‘laana’ ya ukosefu wa album za wasanii wa Bongo Flava

Licha ya kuona kuwa imefanikiwa nje ya mipaka, tasnia ya muziki wa Bongo Flava nchini imegeuka kuwa kama mti wa muembe usiotoa matunda.

c75835b9-b2bf-43e1-ae93-b73d7c264dcd

Ni zaidi ya muongo mmoja sasa utoaji wa album umekufa kabisa. Wasanii wengi licha ya ukubwa wao, wamekubali kuishia kutoa single moja moja, kupata show mbili tatu na maisha yanaenda. Sababu za wao kutotoa album ni za msingi lakini hazimaanishi kusiwepo njia mbadala.

Sababu kubwa ni kutokuwepo kwa wasambazaji wa album hizo pamoja na uharamia wa kazi zao. Lakini uharamia ni kitu ambacho katika nchi zilizoendelea upo katika kiwango cha kutisha lakini hakujawazuia wasanii kutoa album. Uharamia wa huko ni mkubwa kiasi kwamba album ya Beyonce ikitokea leo, ndani ya saa 12 unaweza kuipata yote kwenye tovuti za torrent na ukawa sawa na wale walioinunua.

Wapo wasanii wakubwa hapa Tanzania wenye mashabiki kibao lakini wameshindwa kutumia fursa hiyo kutoa album na huku wakiwa na uwezo wa kuuza nakala 100,000 ndani ya wiki tu.

Nimefurahi sana kuona Navy Kenzo wamepuuzia vitisho hivyo na kuamua kuja na album yao, Above In A Minute inayotarajiwa kutoka mwezi ujao. Kwao, album hiyo inawaweka kwenye ligi tofauti na wasanii wakubwa wa Tanzania ambao bado hawana mpango wa kutoa album zao.

Itawapa heshima zaidi na kuwafanya watembee kifua mbele muda wote wanapokuwa nje ya Tanzania. Wametambua kuwa kwa kadri kundi lao linavyozidi kuwa kubwa, kuwa na santuri iliyoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu watajiongezea CV. Na kitakachoifanya album yao iwe ya pekee, ni muda waliotumia kuiandaa na orodha ya wasanii nguli Afrika waliowashirikisha.

AIM ina dalili ya kuwa album ya uhakika, na sio mkusanyiko tu wa nyimbo zilizowahi kutoka. Uthubutu ambao Aika na Nahreel wameuonesha, unaweza kuwa chachu itakayowaamsha wasanii wengine kuzitoa kabatini lundo la nyimbo wanazoishia kuzisikiliza na washkaji zao na kutoa albums kuwapa zawadi mashabiki.

Kurudi kwa utoaji wa album kutaiongezea nguvu tasnia ya muziki na kuwepo mzunguko mkubwa wa nyimbo nyingi nzuri ambazo hazisiskiki redioni.

Ninawapongeza sana Navy Kenzo wa uthubutu huo na ningeomba watanzania tuwaunge mkono kwa kununua nakala halisi ya album yao.

14574072_326091831107404_4325868722406293504_n

AIM itapatikana kwa shilingi 10,000 tu. Unaweza kuweka oda yako mapema kwa kuwasiliana na.+255 656 762 983.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents