Asilimia 45 ya wanaume wanajijua kuwa wanaishi na maambukizi ya VVU

Asilimia 45 ya wanaume wanajijua kuwa wanaishi na maambukizi ya VVU na asilimia 55 hawajijui huku wanawake waliokuwa wanajijua kuwa wanamaambukizi ni asilimia 56 na 44 bado hawako tayari.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,anatarajiwa kuzindua kampeni ya kitaifa ya Furaha yangu,mkoani Dodoma Juni 19 mwaka huu,inayohusisha upimaji wa VVU na kuanza kutumia ARV.

Hayo yamezungumzwa na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya, Dkt. Angera Ramadhan ikiwa kuwa Kampeni hiyo imetajwa kuhamasisha mkakati wa serikali wa upimaji wa VVU na kuanza kutumia ARV mapema kwa wale watakaokutwa na maambukizi.

“Asilimia 45 ya wanaume wanajijua kuwa wanaishi na maambukizi ya VVU na asilimia 55 hawajijui huku wanawake waliokuwa wanajijua kuwa wanamaambukizi ni asilimia 56 na 44 bado hawako tayari” alisema Dkt. Angera

Dkt. Angera amesema kuwa Kuanza ARV mapema kutapunguza wingi wa VVU mwilini na kuimarisha kinga kwa wagonjwa,hivyo kampeni hii kwa wanaume itakuwa chachu ya kujua afya zao na wengi kuwa tayari kwa kuimarisha afya na kupunguza hatari ya kuambukiza wenza wao.

Aidha Dkt. Angera amesema kuwa serikali itaendelea kubuni mbinu mbadala ili kufikia malengo ya dira ya taifa ya kutokomeza maambukizi ya Ukimwi iliyoridhia malengo ya UNAIDS ya 90-90-90 ambayo ni kuhakikisha asilimia 90 ya watu wote wanaoishi na VVU wanatambua afya zao,wanaanza dawa na kupunguza maambukizi mapya.

Naye Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI TACAIDS, Dkt. Leornad Maboko,alisema uzinduzi wa kampeni hiyo utakuwa na siku tano za kutoa huduma za afya bila malipo,ikiwemo upimaji wa VVU na magonjwa sugu.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW