Habari

Askari augua ghafla, afyatua risasi ovyo

WATEJA wa Benki ya NMB Tawi la Maswa, mkoani Shinyanga wamejikuta wakihaha na kukimbia ovyo baada ya askari polisi aliyekuwa lindoni katika benki hiyo kufyatua risasi ovyo hewani.

na Samwel Mwanga, Maswa

WATEJA wa Benki ya NMB Tawi la Maswa, mkoani Shinyanga wamejikuta wakihaha na kukimbia ovyo baada ya askari polisi aliyekuwa lindoni katika benki hiyo kufyatua risasi ovyo hewani.

 
Watu walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi, sasa 2 asubuhi na kusababisha baadhi ya watu waliokuwa wakisubiri benki hiyo ifunguliwe ili waweze kupata huduma kukimbia ovyo huku wengine wakigongana na kulala chini ili kunusuru maisha yao.

 
Walisema askari huyo, Konstebo Andrew akiwa na askari mwenzake, Konstebo Mwaluko wakiwa katika lindo alianza kumtishia kumshambulia kwa kutumia bunduki aliyokuwa nayo aina ya SMG ndipo walipoanza kunyang’anyana na risasi kuanza kufyatuka.

 
Kwa msaada wa raia, pamoja na askari Mwaluko waliweza kumdhibiti askari huyo na hatimaye kumnyang’anya silaha hiyo na kuchomoa magazine iliyokuwamo.

 
Baadaye askari Polisi wapatao wanne walifika katika eneo la tukio wakiwa na gari PT 0830 na kumchukua askari huyo huku wakiwa wamemfunga kamba kwani alikuwa akiwashambulia kwa ngumi na mateke.

 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Siro Nyankoro, akielezea tukio hilo alisema kuwa ni kweli askari huyo aliugua ghafla akiwa katika lindo hilo ila kabla ya kukabidhiwa silaha alikuwa mzima.

 
Alisema kuwa askari huyo anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa ambako amelazwa na hali yake inaendelea vizuri.

 
Source: Tanzania Daima

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents