Habari

Askari wanafanya kazi kwa gharama ya maisha yao – Waziri Nchemba

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, amesema kuwa Askari wa Jeshi la Polisi pamoja na askari wengine wanafanyakazi kwa gharama za maisha yao, huku akisema kama Taifa tuna wajibu wakutambua kuwa askari wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria.

Hayo yamebainishwa na Waziri Nchemba akiwa Bungeni mjini Dodoma, akijibu hoja za Wabunge ambapo Waziri huyo aliwataka Wabunge kutoa elimu ya vyombo vya dola ili viendelee kupewa heshima inayostahili.

“Askari wetu wa Jeshi la Polisi pamoja na askari wengine ni Watanzania na wanafanyakazi kwa gharama za maisha yao kwahiyo tuna wajibu wa kutimiza kama Taifa kwa kutambua kwa askari wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria na hakuna haki isiyo na wajibu. Sisi kama Jeshi la Polisi eeh Wizara ya Mambo ya Ndani pamoja na taasisi zingine tuna utararibu wakuchukua hatua pindi inapotokea Askari amefanya kazi kinyume na Taratibu,” alisema Mwigulu.

“Lakini vilevile kuna wajibu ambao Watanzania na wananchi kwa ujumla wanatakiwa watimize wajibu wanapokuwa na Askari wetu kwa mfano afadhali sisi ni viongozi wengi wetu tunatoa uongozi tunapokutana na Askari, lakini kuna watu wengine ambao hawatoi heshima inayostahili kwa vyombo vya dola sasa vyombo vyetu vya dola vimepitia mafunzo na mimi kama kiongozi wao nisingependa kuona Jeshi la Polisi linafanana na Green gud, ni lazima Watanzania watambue kwamba vyombo vya dola vina heshima,” alifafanua.

“Lakini ukitaka kupambana na vyombo vya dola wana sehema ambayo wanaruhusu kutumia nguvu wanapoona kile kinachofanya na raia kinaweza hatari ilikuwa zaidi, kwakuwa waheshimiwa wabunge tunakutana na wetu tuendelee kutoa elimu hiyo ili vyombo vya dola viendelee kupewa heshima inayostahili.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents