Habari

Askari watakaogoma kuwapigia saluti wabunge kukiona

Serikali imewaagiza askari wa majeshi yote nchini kuzingatia kanuni za maadili yao ya kazi ikiwemo kupiga saluti kwa viongozi wote wa serikali wakiwemo wabunge.

90c8a860751b252e58c26f97e05856c4_XL

Agizo hilo limetolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole-Nasha wakati akijibu swali kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani [Mwigulu Nchemba] kutoka kwa Mbunge wa viti maalumu Zanzibar, Fakharia Shomari aliyetaka kujua ni kwanini askari wa jeshi la polisi hawapigi saluti kwa wabunge.

Naibu Wazri, Ole Nasha alisema kuwa askari wote nchini ni lazima wazingatie taratibu hizo, na kwamba wanapaswa kupiga saluti kwa wabunge kila wanapowaona, na endapo hawatafanya hivyo, watakumbana na adhabu za kijeshi.

Aidha Naibu Waziri amezitaja baadhi ya adhabu watakazokabiliana nazo askari hao kuwa ni pamoja na kukatwa mishahara yao, kufanya usafi wa mazingira, kuondolewa kikosini kwa muda n.k. Lakini pia amewataka wabunge ambao hawatapigiwa saluti, kuripoti haraka mahali husika.

Hata hivyo Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi amesema agizo hilo linakwenda hadi kwa askari wa makampuni binafsi ya ulinzi ambao mara nyingi hupuuza kutoa heshima hiyo kwa viongozi hususani katika mabenki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents