Tupo Nawe

Aslay aeleza namna alivyoumizwa na mahusiano ‘simtaki mwanamke mwenye tamaa’

Msanii wa muziki, Aslay amedai kwa sasa hataki kukurupuka kuingia kwenye mahusiano ya mapenzi kutokana na matukio aliyopitia kipindi cha nyuma.

Aslay akiwa na mpenzi wake wa zamani

Muimbaji huyo ambaye alikuwa kwenye mahusiano na Tessy na kufanikiwa kupata naye mtoto mmoja, amesema kwa sasa hana mpango wa kuingia kwenye mahusiano.

“Nilishawahi kuumia kwenye mahusiano ya kimapenzi lakini mahusiano hayo hayakuwa kati yangu na mama mtoto wangu Tessy ni ya mwanamke mwingine, ndio maana kwa sasa nipo single,” Aslay alikiambia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.

Aliongezaq,”Sitaki kukurupuka kutafuta mahusino mapya kwa sababu wanawake wengine wanakupenda kwa kuwa ni msanii na wengine wana tamaa”

Muimbaji huyo wiki hii ameachia wimbo wake mpya uitwao, Kwatu ambao umeonekana kupokewa vizuri na mashabiki wengi wa muziki nchini Tanzania.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW