Burudani ya Michezo Live

Aslay na Alikiba waingia studio kuandaa ngoma (Video)

Alikiba ambaye anafanya vizuri na kolabo ya wimbo ‘Nishikilie’ akiwa na Ommy Dimpoz pamoja na Willy Paul ameonekana akiwa pamoja na muimbaji, Aslay hali iliyoibua tetesi huwenda wawili hao wakawa na kazi ya pamoja.

Taarifa hiyo inasambaa katika mitandao ya kijamii lakini yeye mwenyewe bado hawajaweka wazi kama kuna chochote kinakuja licha ya video hiyo kuwaonyesha wawili hao wakiwa busy kurekodi.

Kwa upande wa muimbaji Aslay ambaye anafanya vizuri na wimbo, Chuki ajapost chochote kuhusu ujio wa project hiyo.

Mashabiki katika mitandao ya kijamii wanaonekana kuwa na shauku kubwa juu ya ujio wa project hiyo kutokana na ufundi wa kuimba wa wawili hao.

Naye meneja wa Aslay, Chambuso amethibitisha ujio wa project hiyo ingawa hakupenda kuizungumzia kwa sasa.

Written by Angel Mmasi

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW