Fahamu

Aslay, Vanessa Mdee na Rayvanny ndio wasanii waliosikilizwa zaidi Tanzania kwa mwaka 2018

Wasanii watatu wa Bongo Fleva, Rayvanny, Aslay na Vanessa Mdee ndio wasanii waliosikilizwa zaidi kwenye App ya Boomplay hapa Tanzania kwa mwaka 2018.

Kwa upande wa muziki wa Injili, Joel Lwaga, Martha Mwaipaja na Paul Clement hao ndio nyimbo zao zimesikilizwa zaidi kwa mwaka 2018.

Application ya Boomplay inafahamika kuwa chanzo kikubwa cha ukuaji wa muziki katika bara la Afrika. na mnamo mwaka 2017 boomplay app iliweza kujinyakulia tuzo ya application bora ya muziki barani Afrika kupitia kipengele cha “App Afrika award” ikiwa imewafikia watu million 38 ulimwenguni kote na million 3 kwa Tanzania tu.

Application ya boomplay imeweza kusaidia wapenzi wa muziki kupakua/kusikiliza nyimbo mpya kwa wepesi zaidi lakini pia imeweza kulinda masilahi ya wasanii wetu kwa kuweza kutambua kiasi cha fedha msanii alichoingiza kupitia mauzo ya nyimbo katika kipindi Fulani.

Na kwa mwaka 2018 boompay imezalisha nyimbo million 833 na takribani nyimbo 30,000 zikiwa mbioni kuingia katika application ya boomplay kutoka kwa wasanii mbalimbali na kupitia takwimu za boomplay inaonyesha wasanii kama Vanessa Mdee, Nandy, Jux, Aslay, Mbosso, rayvanny, Harmonize kuwa miongoni mwa wasanii waliosikilizwa zaidi barani Afrika.

Boomplay mpaka sasa imefanikiwa kufanya kazi na makampuni mengine kama vile Universal music, Kudos, Tunicore na Africori na iko mbioni kuzindua application ya iOS.

Kwa wapenzi wa muziki Application ya boomplay inapatikana kiuraisi ikiwa imepakuliwa katika simu za Android kama vile TECNO, Infinix na itel au unaweza kupakua kupitia google play store.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents