Tia Kitu. Pata Vituuz!

Aston Villa hali mbaya Premier League, Samatta anakazi kubwa ya kufanya Villa Park

Klabu ya Aston Villa ipo kwenye kipindi kigumu cha kuhakikisha inaendelea kusalia kunako Premier League hasa kutokana na matumaini kuzidi kwenda mrama.

Mbwana Samatta na mlinzi wa Leicester City, John Evans

Jahazi la Aston Villa linaonekana kuzidi kwenda mrama siku hadi siku kufuatia timu hiyo kupokea kichapo kizito kutoka kwa Leicester City.

Leicester ikiwa katika dimba la nyumbani, King Power, iliwaadabisha Aston Villa kwa magoli 4 – 0 na kuifanya kuendelea kusalia katika nafasi mbaya ya 19 ya msimamo wa ligi, ikiwa na pointi 25 baada ya kucheza mechi 28 wakati Norwich City ikiburuza mkia ikiwa na pointi 21.

Mshambuliaji wa Aston Villa na timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta anayokazi kubwa ya kufanya katika kuhakikisha anaitoa kwenye nafasi hiyo hatari ya kushuka daraja miamba hiyo yenye maskani yake pale Villa Park.

Villa inakabiliwa na michezo migumu kuelekea mwishoni mwa ligi, ikiwa imebakiza mechi 10, ambapo mechi sita kati ya hizo watakutana na vigogo wa ligi hiyo Chelsea, Wolves, Liverpool, Manchester United, Arsenal na Everton.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW