Burudani

At apingana na nyimbo za maombolezi ajali ya meli

at2

Msanii kutoka pande za Zanzibar Ali  Ramadhani Ali maarufu kama AT, amesema yeye hakuona umuhimu wa wasanii wa Zanzibar kuungana pamoja na kutoa wimbo kwaajili ya kuwaomboleza waathirika wa ajali ya meli ya Spice Islanders.

Alisema la muhimu lilikuwa kukutana na kuangalia ni jinsi gani ya kuita wadau wote kwaajili ya kuandaa tamasha la kuchangia fedha kwaajili ya kusaidia waathirika hao, kwakuwa wimbo pekee hautoweza kusaidia kitu.

Alisema kwamba nyimbo ni bora kuimba kwajili ya miaka ya uhuru, kufa kwa mtu mmoja kama kiongozi, na shughuli zingine za kitaifa na sio msiba mzito kama huu.

At alisema yeye alijitoa kwenye nyimbo hiyo na kukaa nje, huku akipanga na Berry Black, kuandaa mfuko kwaajili ya kuchangia wathirika hao , kwakuwa kabla ya hiyo ajali tayari watu Zanzibar wanaishi kwenye maisha magumu, ambayo hata mahitaji ya msingi hawayawezi kuyamudu.

At anasema yeye mwenyewe amefiwa na mama zake wadogo wawili, na wadogo zake watatu kwenye ajali hiyo……………..

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents