Burudani

AT asema anataka kuwa zaidi ya chuo cha mafunzo

AT

Baada ya kurejea kutoka nchini Uingereza msanii wa miondoko ya mduara, AT amekuwa kimya katika maandalizi ya mwanzoni mwa mwaka lakini kesho atatoa wimbo mpya mahsusi kwa wale wenye choyo, kijicho, husda, nongwa, maneno maneno, wambea, roho chafu, kiburi, ngebe, majigambo, hasira za kitamaa na tabia zingine mbaya.

AT ameongea na bongo5 na kueleza kuwa wimbo huo utawahusu watu wenye vitabia vya ajabu kwakuwa mkemeaji wa mambo kama hayo hakuna na yeye amejitolea kuwa zaidi ya chuo cha mafunzo ili wabadilike kwa tabia zao mbaya na waishi kwa amani.

Amesema wimbo huo uitwao “HANA HAYA” utakuwa na muonekano tofauti na umetengenezwa na NK Production chini ya Criss na video itafanywa na Kwetu Studio.

Haya ni baadhi ya mashairi kwenye wimbo huo:

“Kama unataka vita lazima ujiandae, mjini umenikuta kiasi unishangae, Mimi na wewe hatuendani katafute kibanda ukalale, Mimi ni mwema wewe ni jini kazi yako kujichanja machale, ukinitazama ninavyo vutia roho inakuuma unanichuria, ukinitazama ninavyo nukia roho inakuuma unanichuria, hawa ndio wale waliokuja mjini hawana la kufanya hawa ndio wale kazi yao kugombania tu mabwana..!!”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents