Burudani

AT ashinda kesi dhidi ya mganga wa jadi aliyemshitaki

Muimbaji wa Mduara, AT ameshinda kesi iliyokuwa ikimkabili na iliyofunguliwa na mganga wa jadi kwa madai kuwa hakulipwa fedha baada ya kumpandisha nyota na kupata mafanikio mengi.

AT

Akizungumza XXL ya Clouds FM, AT amesema uamuzi huo ni faraja kwake kwakuwa ilimfanya ashindwe kufanya mambo yake.

“Hukumu imetolewa kama dakika tano zilizopita lakini tulikuwa tumefika toka asubuhi saa mbili, kwahiyo itambulike kuwa AT ni msanii huru,” alisema. “Namshukuru Mungu kwa uwezo wake mkubwa kuonyesha waganga wa jadi kwamba yeye yupo na kazi yake ni kubwa na haingiliwi na mtu.

Nimeshinda kwa kishindo kama CCM na sasa najisikia faraja sana, kwa sababu kiukweli kabisa nilikuwa nashindwa kufanya kazi zangu za muziki hata kama nyimbo nzuri basi nahisi hata hii nyimbo ikienda hata kama itafika nitaambiwa nimelogezea hali ya kuwa sio kweli,” aliongeza.

“Pia hata mashabiki zangu nilikuwa nimewaangusha, sasa hivi ndo muda muafaka ndio maana hata nilijifungui ndani nilikuwa nakosa uhuru wa kuishi. Kwahiyo hii kesi imeathiri vitu vingi imenitia nuksi, naacha huu mwaka uishe ili nijipange na mwaka ujao.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents