Michezo

Atakaevunja rekodi hii ajipange – Guardiola

Meneja wa klabu ya Manchester United, Pep Guardiola amewamwagia sifa wachezaji wake na kuwafananisha na wanyama hii ikiwa ni baada ya kuvunja rekodi katika mchezo wao wa hapo jana dhidi ya Swansea.

Meneja wa klabu ya Manchester United, Pep Guardiola

Katika ushindi wao wa mabao 4-0 waliyoupata katika Uwanja wa Liberty unaifanya timu hiyo kuweka rekodi mpya ya kushinda michezo 15 mfululizo na kuvunja ile iliyowahi kuwekwa na Arsenal ya michezo 14.

Nahodha wa Man City, David Silva

Guardiola amewamwagia sifa wachezaji wake kwakuamini kuwa hii ilikuwa ni wiki ngumu kwa upande wa kikosi chake baada ya kutoka kucheza na Manchester United wiki iliyopita kabla ya kuikabili Tottenham siku ya Jumamosi.

“Rekodi hii itakuja kuvunjwa lakini italazimu atakayevunja ajipange siyo kirahisi. Wakati wachezaji wangu wanapokuwa hawana mpira wana haha kama wanyama kwa hatua hii ya ushindani inatoa tafsri kuwa tupo vizuri,” amesema Guardiola.

Kwa ushindi dhidi ya Swansea inatoa tafsiri kuwa City sasa inaongoza katika msimamo wa ligi ikiwa mbele kwa alama 11 nyuma ya Man United.

Guardiola ameongeza “Si rahisi ndani ya siku tatu kwa kile kilichotokea Old Trafford halafu kuwa sawa kimwili na kiakili na kucheza hivi na kuchomoza na ushindi.”

“Katika historia kumewahi kuwa na timu imara kama Liverpool, Manchester United ya Sir Alex Ferguson, na Chelsea ya Jose Mourinho.”

“Kila kitu bora,timu bora hatimae sisi tumekuwa timu ya kwanza kushinda michezo 15 mfululizo na kuwa katika historia. Bilas haka hili halitakuwa namaana kama hatutashinda taji lakini kama hatutoshinda ubingwa itakuwa pia ni rekodi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents