Habari

ATCL na JNIA zapata muwekezaji atakayeleta ndege 8 na mashine za kisasa za usalama

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) pamoja na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam (JNIA) zimepata muwekezaji aliyetoa ahadi ya kuwekeza dola za marekani million mia katika kuboresha huduma.

JNIA

Kwa mujibu wa gazeti la MWANANCHI, Mwenyekiti wa Kampuni ya Maendeleo na Uwekezaji ya Al-Harathy ya Oman, Sheikh Salim Abdullah alitangaza hatua hiyo ya kuwekeza kwenye Uwanja Wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere Dar es Salaam (JNIA) juzi (August 25), kwa kufunga mashine za kisasa na kusisitiza kuwa mashine zilizopo uwanjani hapo kwa sasa uwezo wake kiutendaji na kiusalama ni mdogo.

“Mashine hizi uwezo wake ni mdogo, dunia tunayoishi sasa imetawaliwa na magaidi uwanja wa ndege ni eneo muhimu ambalo linapaswa kulindwa kwa uhakika, mizigo inabidi kukaguliwa kwa umakini zaidi kwani wanaweza kuweka mabomu au vitu vingine vya hatari wakasababisha madhara makubwa alisema na kuongeza”,Alisema

Kwa mujibu wa habari hiyo, Sheikh Salim Abdullah amesema ameitikia wito wa Rais wa Jakaya Kikwete aliyeomba aje kuwekeza, “Nimekuja kuwekeza hapa kwa kuitikia mwito wa Rais Jakaya Kikwete, amechoka sana inabidi sisi tumsaidie, ana nia nzuri ya kuhakikisha nchi hii inakuwa kiuchumi inabidi tumsaidie kuwekeza katika maeneo kama haya” alisema.

ATCL2

Katika hatua nyingine mwekezaji huyo ametangaza kuwekeza ndege nane kwenye Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL), mradi ambao unatarajiwa kugharimu dola za Marekani 100 milioni.

“Tunanunua ndege nane ambapo nne ni aina ya Embraer ERJ-175 za Brazil na nyingine nne aina ya Mbombardier,kwa kuanzia tunapeleka vijana 10 wa kitanzania kwenda kusomea jinsi ya kuongoza ndege hizo” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Kapteni Milton Lazaro, alieleza kuwa hatua hiyo ni faraja kubwa kwao na wana tumaini itatumiwa vyema kwa manufaa ya kukuza uchumi .

Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe alisema Serikali imefanya kazi kubwa kuvutia wawekezaji hao, ikiwa ni pamoja na kusafisha madeni yaliyokuwepo awali.

Picha: Mtandaoni

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents