ATCL, Tutafika kweli??

Ndege ya ATCL aina ya Boeing 737 ikiwa imelalia tumbo baada ya tairi lake la mbele kupasuka wiki iliopita wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa Mwanza. Hakuna majeruhi katika ajali hiyo.

Ndege iliyokuwa na Abiria 39 waliokuwa wakisafiri na Boeing 737 mali ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) jana walikuwa na wakati mgumu baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kunusurika kupata ajali wakati ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza kutokana na kujaa maji.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 1: 47 asubuhi kiasi cha dakika 20 kutoka ilipoanza kutua katika Uwanja wa Mwanza wakati ndege hiyo namba 5H-NBZ ikitokea Dar es Salaam kuingiliwa na maji katika injini yake moja na kusababisha kuzimika na hivyo kupoteza uelekeo na kuvutwa na utelezi wa maji umbali wa mita 400 kutoka eneo lake la kutembelea.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Meneja wa Uwanja wa Mwanza, Muchunguzi Byantao alisema kutokana na hali hiyo rubani wa ndege hiyo Joseph Ibanda alijitahidi na kuiegesha salama kiasi cha kutosababisha madhara na kwamba, hakuna abiria wala mfanyakazi ambaye alipoteza maisha.

“Tukio hili limetokana na maji ya mvua ambayo ilikuwa imenyesha muda mfupi kabla ya kutua, ni kama kipindi cha dakika 20 kutoka ilipotua ndege hiyo, iligonga maji na kuingia katika injini yake moja ambayo ilizima na kusababisha ndege hiyo kuvutwa upande mmoja umbali wa mita 400,” alieleza.

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo ndege hiyo ilipasuka tairi zake za mbele na kujikita katika eneo la nyasi kando ya njia yake na hivyo kukwamia hapo hali ambayo imelazimu kufanyiwa matengenezo na tayari mafundi kutoka Dar es Salaam wameshaitwa.

“Bahati nzuri ndege ilikuwa na wafanyakazi saba na abiria 39 na wote wako salama kabisa, hakuna hata mmoja ambaye ameripotiwa kupata matatizo, isipokuwa hali hiyo ya ndege ambayo itahitaji matengenezo,” alisema kaimu meneja huyo.

Kutokana na ajali hiyo, alisema Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa sasa hautaweza kutumika tena kwa ndege kubwa za aina ya Boeing mpaka hapo ndege hiyo itakapoondolewa na hali ya uwanja kurekebishwa.

 

Wadau hili mnalionaje?

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents