Habari

ATCL wamjibu Mbunge aliyewakosoa wahudumu wao wa kike kukosa mvuto kwa wateja

Baada ya kauli ya Mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), Husna Mwilima kusema kuwa wahudumu wa ndege wanaoajiriwa na Shirika la Ndege Nchini (ATCL) hawana mvuto kwa wateja, Hatimaye ATCL wamejibu kauli hiyo.

ATCL wamesema kuwa hawaajiri wahudumu wa ndege hizo kwa kuangalia sura bali wanaajiriwa kutokana na uwezo wao wa mafunzo wanayopewa.

Hatuchagui wanawake kwa ajili ya kuwapeleka kuonyesha uzuri kuna vigezo lazima tuwapime uelewa. Lazima kujua wana uwezo upi wa kufuatilia mafunzo watakayopewa ili watoe huduma inayotakiwa kwa wateja wetu na si sura,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi.

Jana Novemba 8, 2019 Mbunge huyo akichangia hoja Bungeni Jijini Dodoma, Alisikika akisema “Mheshimiwa waziri mimi nataka nitanie kidogo hizi ndege zetu zinafanya vizuri sana lakini mle ndani hebu tuangalie tunaowaajiri. Wale maair hostess (wahudumu) hata ukimuita mle ndani akigeuka abiria anaona kweli tuna maair hostess mle ndani,” amesema na kuongeza, Sijui mnatumia vigezo gani? Unakuta air hostess mfupi, hana mvuto wa kuifanya ndege zetu zionekane. Leo mimi hapa nimezeeka na miaka 50 na ukiniweka….“.

Chanzo: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents