ATCL yaanza kuingiza ndege

SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) limefanikiwa kununua ndege mbili aina ya bomber dia dash 8, na moja kati ya ndege hizo iliwasili jana majira ya saa sita mchana ikitokea nchini Canada ilikonunuliwa. Kila moja ya ndege hizo, yenye uwezo wa kubeba abiria 50, imenunuliwa kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 8.1 na zinatarajiwa kuliimarisha shirika hilo katika safari zake za ndani.

na Makuburi Ally

 

 

 

SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) limefanikiwa kununua ndege mbili aina ya bomber dia dash 8, na moja kati ya ndege hizo iliwasili jana majira ya saa sita mchana ikitokea nchini Canada ilikonunuliwa. Kila moja ya ndege hizo, yenye uwezo wa kubeba abiria 50, imenunuliwa kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 8.1 na zinatarajiwa kuliimarisha shirika hilo katika safari zake za ndani.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kuwasili kwa ndege hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, David Mataka, alisema Machi 14 mwaka huu, ndege hiyo itapelekwa Afrika Kusini kwa ajili kupakwa rangi halisi za shirika hilo.

 

Mataka alisema kazi ya kupaka rangi nchini Afrika Kusini, itachukuia wiki mbili na mwishoni mwa Machi ndege hiyo itarejea tayari kuanza safari zake hapa nchini.

 

Hata hivyo, kabla ya kuondoka kwenda Afrika Kusini, ndege hiyo itafanya safari za kawaida.

 

“Tunatarajia ndege hii itakwenda Afrika Kusini ambako mwishoni mwa mwezi Machi itaanza kutumia mfumo wa kawaida baada ya kuwa na rangi zake za asili,” alisema Mataka.

 

Aidha, Mataka alisema ndege nyingine ndogo itawasili nchini kati ya Jumamosi na Jumatatu ya wiki ya kwanza ya mwezi Machi na itaungana na ndege iliyowasili jana katika kuimarisha safari za ndani.

 

Mataka alisema safari za ndege hizo zitakuwa ni kwa mikoa ya Kigoma, Tabora, Shinyanga na Zanzibar wakati mara baada ya kufika, ndege kubwa zilizopo, kwa sehemu kubwa zitatumika kwa safari za nje.

 

Alizitaja nchi ambazo ndege kubwa zitafanya safari zake ni pamoja na Afrika Kusini, Dubai kupitia Muscat sambamba na nchi za Malawi, Congo DRC, Zambia, Msumbiji, Rwanda na Burundi.

 

Mataka alisema ndege hizo mbili ni sehemu ya ndege tisa ambazo shirika hilo limepanga kuzinunua zikiwamo tano zenye ukubwa wa kubeba abiria 115 na nyingine nne zenye uwezo wa kubeba abiria 70 kila moja.

 

Mkurugenzi huyo alisema ATCL mwakani imepanga kununu ndege nyingine mbili aina ya Air Bus Q 300 na Q 400 ambazo zitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 74 kila moja.

 

Kuwasili kwa ndege hiyo na ndege nyingine, kunaweza kuwa mwanzo wa kuinuka kwa shirika hilo, ambalo katika miaka ya hivi karibuni, limekuwa likikabiliwa na hali mbaya kiuchumi kutokana na mambo kadhaa.

 

Huu ni mwanzo wa utekelezaji wa mikakati iliyopangwa na menejimenti ya shirika hilo inayoongozwa na wazalendo baada ya kusitishwa kwa mkataba wa ubia baina ya serikali na Shirika la Ndege la Afrika Kusini.

 

 

 

 

 

Source: Tanzania Daima

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents