Michezo

Atletico Madrid kuwavuta Zlatan Ibrahimovic na Diego Costa kikosini

Baada ya klabu ya Manchester United kutangaza kuwa haitamtumia mshambuliaji wao Zlatan Ibrahimovic kuanzia mwakani 2018, Tayari klabu ya Atletico Madrid imetangaza kumhitaji mchezaji huyo ili kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.

Diego Costa na Zlatan Ibrahimovic

Klabu ya Atletico Madrid ambayo imezuiliwa na FIFA kufanya usajili kwa msimu huu itamchukua Zlatan pindi atakapopona majeraha yake mwakani huku ikimsubiria Diego Costa ambaye msimu huu anaihama klabu ya Chelsea baada ya kocha wake Antonio Conte kusema hatamtumia msimu ujao.

Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania tayari Klabu ya Atletico Madrid imeshafanya mazungumzo na Diego Costa na kukubaliana kuwa mchezaji huyo aondoke Chelsea kwa mkopo kwenda klabu yoyote ile mpaka Atletico watakapomaliza adhabu yao januari mwakani ndipo watamsajili.

Diego Costa ambaye alitakiwa kusajiliwa na Atletico Madrid msimu huu kwa masharti ya kubaki nje ya uwanja mpaka mwakani amekataa kufanya hivyo kwani amedai anahitaji kucheza kwasasa ili kujihakikishia namba kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kuelekea michuano ya fainali ya kombe la dunia 2018.

Atletico wamefikia hatua ya kumuhitaji Zlatan kwenye usajili wa dirisha dogo januari mwakani ili aweze kuiongezea timu hiyo makali wakati wakiendelea kumsubiri Diego Costa.

Zlatan ambaye yupo nje ya uwanja akiuguza majeraha hakuna klabu nyingine kubwa iliyoonesha nia ya kumsajili Msweden huyo .

By Godfrey Mgallah

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents