Michezo

Atokwa na meno baada ya kumng’ata golikipa

Beki wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Godin hapo jana siku ya Jumapili alijikuta akitokwa na meno baada ya kumng’ata golikipa wa Valencia katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania Laliga.

Klabu hiyo ya Atletico imetoa taarifa kuwa Godin amefikishwa katika hospitali ya meno jijini Madrid  kufuatia dhahama hiyo huku timu hiyo ikiibuka na ushindi wa bao 1 – 0 katika dimba la Wanda Metropolitano.

Baada ya tukio hilo ililazimika Godin afanyiwe mabadiliko haraka mapema mwa kipindi cha pili cha mchezo huo huku wakati tukio hilo likiwa limetokea wakati mlinda lango wa Valencia Neto akiokoa mpira wa hadhabu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents