Uncategorized

Aubameyang ang’ara mbele ya Burnley, ampiku Mo Salah kwa mabao EPL

Straika wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang amefanikiwa kufunga jumla ya magoli mawili katika ushindi wa mabao 3 – 1 dhidi ya Burnley kwenye mechi ya ligi kuu Uingereza iliyopigwa leo dimba la Emirates.

Pierre-Emerick Aubameyang celebrates with Alexandre Lacazette

Magoli hayo mawili ya Aubameyang yamemfanya kufikisha idadi ya mabao 12 na hivyo kuongoza katika msimamo wa wanao wania kiatu cha dhahabu msimu huu akimpiku Mo Salah mwenye 11.

Nyota wa Burnley, Ashley Barnes akifunga bao la kufutia machozi kwa upande watimu yake huku dakika za lala salama Alex Iwobi akihitimisha karamu hiyo yamabao na kuifanya kuamka baada ya kupoteza michezo miwili iliyopita huku Mesut Ozil akirejea tena kwenye nafasi yake ya unahodha.

ArsenalLeno (6), Sokratis (6), Elneny (6), Monreal (5),Maitland-Niles (6), Xhaka (6), Guendouzi (6), Kolasinac (8), Ozil (7),Lacazette (6), Aubameyang (8)

Wachezaji wa akiba, Lichtsteiner(6), Torreira (5), Iwobi (6)

Burnley: Hart (6), Bardsley (5), Tarkowski (5), Mee (5),Long (6), Taylor (6), Cork (6), Westwood (5), Hendrick (5), Barnes (6), Wood (5)

Wachezaji wa akiba: Vydra (5), Vokes (5), Lowton (n/a)

Man of the Match: Sead Kolasinac

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents