Michezo

Aubameyang avunja rekodi ya magoli kwenye Bundasliga

Mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang amevunja moja ya rekodi za uchezaji soka nchini Ujerumani.

160113151647_pierre-emerick_aubameyang_512x288_ap_nocredit

Mchezaji huyo kutoka Gabon ndiye mchezaji kutoka Afrika aliyefunga mabao mengi zaidi katika ligi kuu ya soka ya Ujerumani Bundesliga msimu mmoja.

Aubameyang, ambaye alitawazwa mchezaji bora wa mwaka 2015 Afrika wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) alifunga bao lake la karibuni zaidi dhidi ya Werder Bremen Jumamosi na kufikisha 23, idadi ya mabao aliyofunga msimu huu.

Rekodi ya awali ilikuwa ya mabao 22 na iliwekwa na Cisse Papiss wa Senegal msimu wa 2010/11 ambaye kwa sasa anachezea timu ya Newcastle United ya Uingereza.

Msimu huu wa 2015/16 pia, Aubameyang alikuwa ameweka rekodi kwa kufunga bao katika kila mechi mechi nane za kwanza za msimu wa Bundesliga, akiipita rekodi ya awali kwa mechi mbili.

Kwa kuwa alikuwa amefunga mabao mechi mbili za mwisho za msimu wa 2014-15, alivunja rekodi nyingine ya kufunga mabao mfululizo katika mechi 10 za Bundesliga. Mtu pekee aliyekuwa ameifikia ni Klaus Allofs miaka 30 iliyopita.

Source: BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents