Habari

Audio: Alberto Msando ateuliwa nafasi hii ACT wazalendo

Chama Cha ACT- Wazalendo kimemtangaza rasmi Mwanasheria, Albert Msando kuwa Mshauri wa masuala ya sheria wa Chama hicho.

Akizungumza na Bongo5 Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi, Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema uteuzi huo umeanza tarehe 7 na kutangazwa leo kutokana na sababu zilizokuwa nje ya chama hicho.

“Chama cha ACT Wazalendo kimefanya mageuzi makubwa ya kiuongozi, ukiachilia mbali kiongozi wa Chama na Mwenyekiti wa Chama, viongozi wengine wote waliobakia chini wamefanyiwa mabadiliko, kwa hiyo moja ya mabadiliko hayo ndugu Albert Msando ambaye alikuwa mwanasheria Mkuu wa Chama, alikuwa mwenyekiti wa sheria, sasa amefanywa kuwa Mshauri Mkuu wa masuala ya Kisheria. Hii ni tofauti na ya Profesa Kitila Mkumbo yeye alikuwa ni msahauri wa jumla ya chama kwahiyo Msando ni Mshauri wa masuala ya Kisheria,” amesema Shaibu.

Uteuzi huo ulianza rasmi tarehe 7 May 2017

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents