Habari

Audio: Cindy Rulz auelezea wimbo wake ujao, ‘Let’s Wait’ aliomshirikisha Dunga

Rapper wa kike wa Fish Crub, Cindy Rulz, anatarajia kuachia wimbo mpya uitwao ‘Let’s Wait’ aliomshirikisha producer Dunga ambaye ameshirikiana na Lamar kuutengeneza.

photo 1

Akiongea na Bongo5, Cindy amesema ‘Let’s Wait’ ni wimbo wenye mahadhi ya Hip Hop na RnB na ni wa mapenzi.

“Ni kama msichana anakuwa anamuambia bwana yake kwamba kwa sasa hivi hawawezi kuwa kwenye mahusiano. Japokuwa kwamba anamfeel jamaa lakini kwasababu ya masomo, mazingira ya nyumbani vitu kama hivyo vinakuwa vinamzuia kabisa kuingia kwenye uhusiano,” amesema.

Cindy amesema awali beat ya wimbo huo ilikuwa na sample ya ngoma ya Janet Jackson na hivyo wakati wa kutaka kuuandikisha kwenye mamlaka husika akakutana na kikwazo kutokana na kuambiwa awasiliane na Janet ili ampe ruhusa kutumia kionjo hicho.

“Sasa nikafikiria in reality mpaka nimpate Janet Jackson design inakuwa very untrue,” amesema.

Ameongeza kuwa ilibidi amuambie tu Lamar waupotezee wimbo huo na wafanye mwingine.

Lakini wakati anamuambia hivyo Lamar, Dunga alikuwepo na akamwambia kuna uwezekano wa kutengeneza beat nyingine kabisa kwakuwa aliupenda wimbo huo na hakutana upotee. Baada ya Dunga kutengeneza beat nyingine, walishauriana wamtafute mtu wa kufanya chorus lakini Cindy alihofia kuwa inaweza kuchukua muda mrefu mpaka kumpata mtu atakayefanya chorus bila usumbufu na hivyo Dunga kuamua kuimba kionjo cha chorus ili Cindy afuatilize kwa juu.

“Nikasema hiyo inawezekana lakini haitasound vile navyotaka mimi. Kwahiyo ‘kwanini usijaribu kufanya wewe kama wewe’. Na kweli (Dunga) akaingia kwenye booth, akafanya yake and it turned out amazing,”ameongeza Cindy.

Cindy anasema ‘Let’s Wait’ ni wimbo tofauti na zile alizofanya mwanzo kwakuwa ameuvaa uhalisia zaidi.

Msikilize hapa.

[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/117619287″ width=”100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents