Burudani

Audio: Diva kwenda kufanya video ya ‘Jicho la Huba’ Afrika Kusini

Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Loveness aka Diva the Bawse amesema atakwenda kufanya video ya wimbo wake mpya, Jicho la Huba nchini Afrika Kusini. Kwenye wimbo huo Diva amewashirikisha Gosby na Stereo.

a239573822c911e3838b22000ae81190_7

Akiongea na Bongo5, Diva amesema ameamua kwenda kufanya video hiyo nchini humo kwakuwa anataka kufanya video yenye kiwango cha juu zaidi na pia nchini humo kuna location nzuri.

“From the beginning nilisema if not South Africa ni Kenya so the problem with Kenya ni kwamba kuna Al-Shabaab. Kiukweli I am really scared about Al-Shabaab. So naenda kufanya South Africa, everything is under control, I mean the budget, jinsi ya kufika kule, kukaa kwenye hotel gani, mpaka kumaliza,” amesema Diva.

“If Stereo na Gosby watakuwa na nafasi pia tutaenda nao South Africa, there is no problem with that, I can afford paying I can afford paying for them.”

Akijibu la swali kuhusu ni wapi anapata fedha za kuweza kumudu gharama hizo, Diva amesema: I am working, mimi nafanya voice over, apart from me being the radio personality nina kazi yangu mimi nafanya, nina kampuni na I get money so I can afford kwenda South Africa, go and return, I can afford kulipia watu, I can afford ku’make sure nakuwa na video nzuri.”

Diva amesema anafikiria kuitumia kampuni ya Ogopa ya Kenya ama Nisher kwaajili ya kufanya video.

Msikilize zaidi hapa.

[soundcloud url=”http://api.soundcloud.com/tracks/112772667″ params=”” width=” 100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents