Burudani

Audio: Joh Makini aielezea maana ya style ya Weusi waliyoibatiza jina la ‘Viburi Flow’

Hivi karibuni rapper wa kampuni ya Weusi, Joh Makini na Nikki wa Pili walitambulisha style yao mpya ya rap, iitwayo ‘Viburi Flow’.

604039_10151323274983598_314045081_n

Akiongea na Bongo5 hivi karibuni, Joh Makini alisema waliamua kuanzisha flow hizo ili kujitofautisha na rappers wengine na kufanya nyimbo zao zisiwachoshe watu.

“Utakapotusikia sisi, utagundua kuwa tunapiga michano tofauti na marapa wengine nchi,” alisema Joh. “Marapa wengine wamekuwa wakipiga flow moja since wameanza kutoka kwenye game. Kwahiyo sisi ili kuleta changamoto na kupanua sura ya huu mchezo, tumeamua at least katika verse moja mtu unakuwa unapiga miondoko hata mitatu tofauti ili kusudi usimboe msikilizaji ambaye anaendelea kusikiliza. Sababu toka 2006 mpaka leo ningekuwa na flow moja tu, hata kama ningekuwa nakuja na kitu gani kingine ninachowaambia watu, wangeona ‘aahhh’. Uemcee ni zaidi ya uandishi. Lazima uwe na kitu tofauti katika michano yako ili kuwafanya watu waendelee kukusikiliza, kila siku uwe mpya ndio maana tukaanzisha hii Viburi Flow. Tunapiga flow fulani mpya ambazo hazijawahi kupigwa kwenye hii game.”

Joh aliongeza kuwa jina la style hiyo lilikuja tu wakati walipokuwa wakirekodi wimbo na producer Dunga.

“Ilikuwa siku moja nafanya kazi na Dunga studio, nikapiga akaniambia ‘man hizi flow zina confidence mbaya, yaani Viburi Flow’, basi ndio ikaanzia hapo.”

[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/118216022″ width=”100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents