Burudani

Audio: Jokate Mwegelo azungumzia birthday yake na namna alivyobarikiwa

Ni ngumu kuitawala Instagram au Twitter kwa salamu za siku ya kuzaliwa labda kama ukiwa Jokate Mwegelo.

Jokate Mwegelo

“I feel very blessed kusema ukweli, nasikia nimebarikiwa sana, watu wananijali, wananipenda, wananikumbuka kwenye siku yangu muhimu ya leo na wananipost kwenye Instagram, namshukuru Mungu,” Jokate ameiambia Bongo5. “Baadaye I may have dinner with some good friends, close friends, a dinner party, some good nini,” ameelezea namna atakavyoisherehekea siku yake ya kuzaliwa leo.

Jokate amesema ni ngumu kutaka idadi ya Baraka alizozipata, lakini amesema mpaka anasherehekea leo siku yake ya kuzaliwa, ni mengi aliyofanikiwa. “Everything kwangu mimi ni achievement lakini obviously I keep on working hard for even better thing,” amesema.

Jokate pia amewashukuru mashabiki wake ambao wamekuwa wakimtia moyo na kumpa nguvu ya kujituma zaidi.

Happy Birthday Kidoti. Msikilize zaidi hapo chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents