Muziki
Audio: Makamua aachia ‘Mission Impossible’ aliomshirikisha staa wa Angola, Linda
Mkali Kwanza, Mark Paul aka Makamua leo ameachia wimbo uitwao ‘Mission Impossible’ aliomshirikisha msanii wa nchini Angola, Linda Innes.
“Kitu ambacho nimewasurprise ni kwamba nimerudi na Makamua yule waliyekuwa wanamsikia,” Makamua alikimbia kipindi cha Kali za Bomba cha Bomba FM, Mbeya.
“I sound African, Tanzanian R&B is back. Linda Innes ni Coca-Cola pop star namba moja wa Angola.”
Msikilize hapa akiuongelea wimbo huo.
Makamua amesema msanii huyo alikuja Tanzania pia atafanya nyimbo kadhaa na wasanii wa Tanzania wakiwemo Lady Jaydee na Profesa Jay.