Burudani

Audio: Profesa Jay amuezi marehemu mama yake kwenye ngoma mpya ya JCB ‘Drive Slow’

Profesa Jay ametumia wimbo wa JCB, Drive Slow kumuemuenzi marehemu mama yake Bi. Rosemary Majanjara aliyefariki mwanzoni mwa July mwaka huu kwa kugongwa na gari.

1045258_10151532026058517_258883389_n
Marehemu mama yake na Profesa Jay

Katika wimbo huo ambao Profesa Jay ameshirikishwa, JCB na Jay wanatoa ushauri kwa madereva wa magari kuendesha kwa mwendo wa taratibu kuepusha ajali.

“Ajali wewe ndiye uliyemchukua mama yetu mpenzia/alipokuwa akivuka barabara maeneo ya Mbezi/tunamiss upendo wako na tunakuombea kwa mwenyezi/na mama pumzika pema daima tutakuenzi/dereva hebu simama pale unapoona zebra/ona umemgonga mama na maisha ameyapoteza,” anarap Jay.

Kwenye wimbo huo, Profesa pia anagusia pia jinsi familia yao ilivyoumia baada ya dereva wa gari iliyomgonga kuachiwa huru.

“Kinachotuuma zaidi eti sheria imemwachia/daima tutakulilia , muuaji hana hatia?”

Sikiliza kionjo cha wimbo huo hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents