Habari

Audio: Rais Magufuli ampigia simu mwanamke aliyemwagiwa uji wa moto na mumewe

Rais Dkt John Pombe Magufuli, amempigia simu mwanamke aliyemwagiwa uji wa moto na mume wake huko Mara.


Neema Mwita Wambura akizungunza Rais Magufuli na kumshukuru kwa msaada aliompatia wa kufanyiwa tena uchunguzi wa afya yake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Neema Mwita Wambura (32) alimwagiwa uji wa moto ukiwa unachemka jikoni na mume wake katika kijiji cha Kyagata,Tarime mkoani Mara baada ya mume huyo kukasirika kwasababu Neema alichuma mahindi mabichi na kuyapika bila kibali cha mumewe.

Baada ya hapo majeraha yamekuwa yakimsumbua mno katika mwili wake.

Rais Dkt John Magufuli aliingiwa na huruma baada ya kumuona Neema, na alimpigia simu pamoja na kuwaagiza watu kumpatia fedha za matibabu pamoja na kumjulia hali yake.

https://youtu.be/FGjiTJPHspA

Rais Magufuli ameahidi kumpatia hifadhi mama huyo pamoja na watoto wake watatu ambao kwa sasa wapo Bunda mkoani Mara. Pia alimpatia msaada wa shilingi laki tano.

By: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents