Audio: Shaa asema na baba wenye nyumba ‘wanoko’ kwenye Baba Kodi

Asilimia kubwa ya wananchi huanza maisha kwa kupanga kwenye nyumba ambapo kutokana na uwezo wa kila mpangaji, wapo wanaopanga kwenye chumba kimoja, viwili nk na wengine wakichukua nyumba nzima.

shaa

Kwa bahati mbaya wapangaji wengine wamejikuta wakipanga kwenye nyumba za wamiliki wasumbufu na wanoko ambao hudai pesa yao ya pango kwa usumbufu mkubwa na hao ndio Shaa ameamua kuwapa ujumbe wao kwenye Baba Kodi.

Kwa wapangaji wenye vifua vipana Baba Kodi ni wimbo mzuri kuupiga kwa sauti ili baba/mama mwenye nyumba mwenye tabia hii aweze kuupata ujumbe. Ni wimbo ambao pamoja na kuwa na ujumbe mzuri, unachezeka pia na kuufanya uwe 100% club banger.

Wimbo umetengenezwa na Manecky wa AM Records. Enjoy.

Download Hapa

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents