Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Audio: Sina mpango wa kuhamia CCM – Mh. Kubenea

Mkurugenzi wa Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL) na Mbunge wa jimbo la Ubungo,(Chadema) Saed Kubenea amesema hana mpango wowote wa kuhama Chama chake cha Demokrasia na Maendelea(CHADEMA) na kuhamia CCM kama inavyodaiwa mtandaoni.

Kubenea ameiambia Bongo5 leo, kuwa wananchi wanapaswa kupuuza taarifa hizo kwani yeye ataendelea kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama chake.

“Nadhani ni udhaifu wa watu kwasababu kama mtu anaandika taarifa kwamba Mbunge ana hama na aliyeandika taarifa hizo ni Mbunge bila kumuuliza Mbunge mwenzake bila kuwasiliana nae hiyo ni shida me naona is not fair,” amesema Kubenea.

“Wananchi wapuuze taarifa zozote zinazonihusisha mimi na kuondoka Chadema na kujiunga na CCM hizo ni za Uzushi mimi bado ni mwananchama wa Chadema na bado ni Mbunge wa Ubungo na sina mpango huo na sijawahi kuzungumza na mtu yoyote.”

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW