Burudani

Audio: Tulichowekeza kwa Rich Mavoko bado hakijarudi hata robo – Sallam SK

Meneja wa WCB, Sallam SK amefunguka kwa kudai kwamba pesa ambayo wamewekeza kwa msanii Rich Mavoko bado haijarudi huku akidai hata yeye hajui kitu ambacho kimemfanya muimbaji huyo kwenda kulalamika Basata.

Muimbaji huyo ambaye yupo chini ya WCB, wiki iliyopita alienda Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kulalamikia mkataba wake aliosaini na label hiyo kubwa ya muziki nchini Tanzania.

Akiongea na The Playlist ya Times FM Jumatano hii, Sallam SK amedai kwamba mpaka sasa pesa ambayo wamewekeza kwa muimbaji huyo katika project zilizotoka haijarudi hata robo.

“Pesa ambayo tumekeza kwa Rich Mavoko haijarudi hata robo,” alisema Sallam.

Related Articles

29 Comments

  1. Mkataba huwa ni makubaliano kati ya pande mbili au zaidi na kila upande huwa unasoma/kusikiliza vigezo na mashariti vya mkataba kisha ndo unatia sign. Na ikitokea upande mmojawapo ukakiuka mkataba basi uko responsible kulipa gharama na usumbufu utakaojitokeza.Kwa hiyo kama #RuchMavoko anataka kuvunja mkataba awe tiyari kulipa gharama zote.

  2. Unalikumbuka la zari na mond kuachana!?
    Mwisho wa cku watu wakashangaa mtu wamuona kwny kichupa cha mond tena wakat ilivuma, ooh mond na zari ndo basi ‘umeona upuuz wao hawa watu…

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents