Burudani

Audio: Utani Utani ni kama tukio la Tundu Lissu, kauli za Rais Magufuli – Young Dee

Msanii wa muziki kutoka label ya King Cash, Young Dee amefunguka kwa kudai kuwa wimbo wake mpya ‘Utani Utani’ ni zao kutoka katika maamuzi ya Rais Magufuli pamoja na ugomvi ambao uliibuka kati ya Diamond na Ommy Dimpoz.

Akiongea na Bongo5 Jumatano hii kwa njia ya simu akiwa mkoani, Young Dee amesema wimbo huo ameuandika kutokana na matukio ambayo yanatokea kiutani na baadaye kuibuka kuwa ndio habari ya mjini.

“Nimejaribu tu kuelezea “Utani Utani” ambao unaweza kuleta shida, kwa mfano hivi karibuni kuna hawa ndugu zetu (Diamond na Ommy Dimpoz) walikuwa wanataniana lakini wakavuka mipaka mpaka watanzania wakachukia, kwa sababu walianza kuzungumza mpaka mambo ya ndani, ni Utani ambao unaweza ukafanya mpaka sisi tukashindwa kuongea,” alisema Dee.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents