Burudani ya Michezo Live

Audio: Victoria Kimani awashirikisha kaka zake Bamboo na Kimya katika wimbo mmoja ‘Trayvon’

Mstaa ndugu wa familia moja kutoka Kenya rapper Bamboo na Kimya wameshirikishwa na dada yao mwimbaji Victoria Kimani katika wimbo wake mpya ‘Trayvon’ kutoka katika mixtape yake mpya ‘Queen Victoria’.

vicbamkim

Trayvon ni sample ya wimbo wa Drake ‘Started from the Bottom’ na Victoria ameutoa kama dedication kwa kijana mwenye asili ya Afrika Trayvon Martin wa Miami, Florida aliyefariki kwa kupigwa risasi nchini Marekani.

Ni wimbo uliobeba ujumbe unaohusiana na maswala ya ubaguzi wa rangi na umasikini unaowalenga Waafrika hasa waishio Marekani.

Katika wimbo huu Victoria ameimba chorus na kaka zake Bamboo na Kimya wamezishambulia verse.

Victoria ambaye alizaliwa Marekani hivi sasa makazi yake ni Nigeria ambako ndiko anafanyia shughuli zake za muziki. Rapper wa muda mrefu Bamboo hivi sasa anafanya muziki wa gospel toka aokoke.

Sikiliza hapa

Source: Niaje

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW