Habari

AUDIO: Walichokisema wazazi wa Akwilina baada ya mazishi ya mtoto wao

Wazazi wa marehemu Akwilina Akwilini Bafta wamefunguka baada ya mazishi ya mtoto wao huyo ambayo yalifanyika jana (Ijumaa) katika eneo la nyumbani kwao, katika kijiji cha Marangu Kata ya Marangu Kitowo wilaya ya Rombo, ambapo Serikali kupitia Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako waliongoza maelfu ya Watanzania katika ibada maalum ya kuuaga mwili huo.

Akiongea na Bongo5, Baba mzazi wa Akwilina, ameishukuru Serikali pamoja na Watanzania waliojitokeza katika kuuaga mwili huo pamoja na ushirikiano huku akiwaomba Watanzania kwa ujumla kuzidi kumkumbuka.

Hata hivyo Mama Mzanzi wa marehemu alipohojiwa na Bongo5 ameshindwa kuongea lolote huku machozi yakizidi kumtoka kwa uchungu akisema hana neno lolote la kusema.


Baba na Mama mzazi wa akwilina wakiweka shahada la maua kwenye kaburi la mtoto wao

Hali ya usalama nyumbani kwa kina Akwilina kuliimarishwa na ulinzi wa kutosha kwasababu ya wingi wa watu waliojitokeza kumuaga binti huyo wakati vilio na simanzi vikitawala katika kijiji cha Marangu.

Kwa upande wa Serikali msafara wake uliondoka nyumbani kwa wazazi wa marehemu baada ya mazishi hayo yaliyofanyika majira ya Alasiri na kuwaacha baadhi ya wafiwa nyumbani kwao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents