Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Audio: ZaiiD ataja sababu ya kumtumia Mafuru na sio Mecky kwenye ‘Wowowo’

Rapper ZaiiD anaye wakilisha kundi la Hip Hop Bongo la SSK, ametaja sababu za kumtumia director Mafuru katika video yake ya ‘Wowowo’ iliyotoka wikiendi iliyopita.

Akipiga stori na Bongo5, rapper huyo ameeleza kuwa amemtumia Mafuru kwani ameona ndiyo anafaa katika video hiyo na amempumzisha Mecky Kaloka coz anavideo zingine zinamfit.

” Mecky ni mtu ambaye tunafanya naye kazi mara nyingi sana kati ya video tunazofanya naye ni zile video za battle, kwa mimi binafsi nam-consider ni mtu ambaye anafanya video za really Hip Hop,” amesema ZaiiD

Akaongeza “Hii ni kwa sababu trak inahusisha mapenzi espicially inamuhusu binti, nikaona kuwa Mafuru anafit sana na nishaona baadhi ya kazi nikaona ngoja nimcheki nifanye naye kazi tofauti na nifanye video yenye taste tofauti.”

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW