Burudani

Audio/Video: Rita Paulsen kwenye Chill na Sky

Wiki hii kwenye Chill na Sky, @skytanzania amechill na Rita Paulsen, @mspaulsen na kuchat issue kibao kuanzia maisha yake akiwa mdogo, kazi zake za kwanza kufanya zikiwemo modelling, alivyoanzisha kampuni ya Benchmark Productions, namna alivyoset standards za video za muziki Tanzania kwa kutengeneza video ya kwanza ya @jidejaydee ya wimbo wake Machozi, video ya Zali la Mentali ya @ professorjaytz f/ Juma Nature.

Amezungumza pia jinsi mwanzoni alivyokatishwa tamaa kwa wazo lake la Bongo Star Search, alivyotumia miaka mitatu kusaka mdhamini bila mafanikio, jinsi ambavyo alipata mshtuko mkubwa kuona mahudhurio ya kutisha kwenye audition ya kwanza kabisa jijini Dar es Salaam.

Sikiliza kipindi kizima hapo chini.

Amezungumzia pia jinsi ambavyo alimuongeza Salama Jabir, @ecejay ambaye alishawishiwa naye baada ya kuidiss video ya muziki iliyoongozwa na kampuni ya Benchmark Productions. Ameongelea pia msimu mpya wa shindano la @bongostarsearch.

Chill na Sky inasikika kupitia Kings FM ya Njombe (Jumatatu 10:45 hadi 11:45 jioni, na marudio Jumapili saa 5:00 asubuhi. Bomba FM Mbeya, Jumanne saa 9:00 Alasiri na Afya Radio 96.8, Mwanza, Jumatano saa 8:30 mchana kwenye The Beat Lab na kurudiwa Ijumaa saa 5:00 usiku kwenye Weekend Jump off na Jumapili saa 5:00 asubuhi kwenye Super Sunday.

Chill na Sky ni product ya Bongo5 Media Group!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents