Michezo

Aumia vibaya wakati akishangilia bao lake

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Hamburg, Nicolai Muller amejikuta akiingia katika majeraha  baada ya kusherekea bao lake alilofunga dhidi ya Augsburg siku ya Jumamosi.

Muller alifunga bao hilo kunako dakika ya nane ya mchezo huo na kuruka hewani kwa furaha kisha kuanguka vibaya hali iliyoonyesha kupata machungu sana katika mwili wake kabla ya wachezaji wenzake kumkimbilia kumpa msada.

Kocha wa kikosi cha Hamburg, Markus Gisdol amesema kilikuwa kisa cha kushangaza.

Mchezaji huyo aliumia sehemu za goti la kulia na hivyo kukaanje kwa miezi saba akiuguza jeraha lake wakati Mkurugenzi wa michezo wa kalbu hiyo, Jens Todt amesema.

“Uchunguzi wa jeraha lake ulitushangaza, ni pigo kubwa sana kwetu mwanzo wa msimu na bila shaka pigo kubwa zaidi kwa Nicolai.Twamtakia apone haraka na tutamsaidia kadiri ya uwezo wetu”.

Muller mwenye umri wa miaka 29, alijiunga na Hamburg akitokea Mainz mwaka 2014.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents