Burudani

Aunt Ezekiel adai wasambazaji wanaua soko la filamu Tanzania

Aunt Ezekiel amesema wasambazaji wa filamu ndio watu wanaoliua soko la filamu Tanzania.

11881690_1469293913374561_1521758061_n

Akiongea kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV hivi karibuni, muigizaji huyo alisema msambazaji yupo tayari kununua kazi mbaya kwa bei ya chini na kuacha kununua kazi ambazo zimeandaliwa vizuri.

“Msambazaji mhindi yaani sasa hivi amefikia hatua yupo radhi anunue kazi ambayo ataona kwenye cover tu labda yupo Aunt au staa mwingine ilimradi kwenye cover yupo hata akiwa hajacheza sana kwa bei nafuu zaidi ili asije akanunua filamu ya Ray kwa bei kubwa lakini ni bora na imeandaliwa vizuri,” alisema.

“Sasa mtu anayekwenda kununua akiona msanii alichokifanya kule kwenye kazi ambayo umeonekana mara moja ni mbaya, anavyokuja kuona cover ya filamu mpya ya Ray anajua ndio yale yale, hakuna jipya, kiasi kwamba watu wamekuwa wamechoka vile vile.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents