Michezo

Aussems ‘Uchebe’ alivyouchukulia mchezo wa Sevilla FC ‘Ilikuwa Show Time/ndiyo maana kila mchezaji nilitaka apate nafasi / tumewatikisa’ (+video)

Mara baada ya kukubali kipigo cha mabao 4 – 5 kutoka kwa miamba ya soka ya Hispania, Sevilla FC, Kocha Mkuu wa klabu ya Simba, Patrick Aussems amesema hayo matokeo kwake hayamuumizi kichwa kwakuwa aliwatoa wachezaji wake tegemezi dakika 45 za kipindi cha pili ili kupisha wengine nao waonyeshe uwezo wao na kupata kuonekana kwakuwa ilikuwa ni mechi ya kirafiki ambapo kwake alitumia neno ‘show time’.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mechi hiyo kubwa na ya kirafiki, Aussems amesema ”Nafikiri mnafahamu kilichotokea, nilifanya mabadiliko yasio ya lazima kwasababu haukuwa mchezo muhimu bali ni ‘show time’, nilihitaji wachezaji wote wapate nafasi ya kushiriki na kuonekana na kucheza na moja kati ya timu bora barani Ulaya.” amesema Aussems.

Patrick Aussems ameongeza kuwa ”Ndiyo maana nikafanya mabadiliko mengi ya wachezaji, kuwafanya wao wawe na furaha kwasababu pia mmeona timu ilitikisika mmeweza kujionea dakika za mwisho, kwahiyo ilikuwa mchezo mzuri, msisahau kuwa tumekuwa mabingwa siku mbili zilizopita. Ilikuwa mechi nzuri kupata kuwafunga magoli manne Sevilla FC kwangu naweza kusema tumefanya vizuri.”

”Mnafahamu niliwaambia wachezaji kuwa ni show time, hata wao wamemaliza ligi siku chache zilizopita na wamekuja hapa kama ‘hollydays’ na tumewatikisa na nafikiri hawakutarajia na ndiyomaana tulivyowaongoza kwa mabao mawili (2 ) walirudi tena na kutaka kutuonyesha kuwa wao ni Sevilla FC wakapata bao moja na ni kutokana na makosa yetu ila vyote ni kawaida.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents