DStv Inogilee!

Avril (Kenya) aishindwa style ya AT, collabo yashindikana

Avril Nyambura

Mwanamuziki wa kike wa nchini Kenya, Avril Nyambura hivi karibuni ameshindwa kumridhisha AT kwa kiwango chake cha uimbaji baada ya msanii huyo mahiri kwa mduara kutaka kumpa collabo.

Akiongea na Bongo5, AT amesema alisafiri hadi jijini Nairobi na kukutana na Avril kwenye studio za Ogopa DJ, na kumwandikia mashairi na melody msanii huyo ambazo hata hivyo zilimshinda kuziimba.

AT

Ameongeza kuwa pamoja na kurudia sana sauti hizo, Avril alishindwa na hivyo AT aliamua kumpa muda zaidi wa kuifanyia mazoezi ili aje kuifanya baadaye lakini hata hivyo kazi hiyo haikufanyika tena.

Awali AT amedai alikuwa amepanga kufanya wimbo na Juliana wa Uganda na alienda kumtafuta hadi nchini kwake lakini hakufanikiwa kumpata.

Amesema imembidi amtafute msichana aitwaye Alice wa THT ambaye ameweka vionjo vizuri zaidi kuliko alivyokuwa akitegemea.

Wimbo huo anaosema una mahadhi ya zouk classic utatoka mwezi ujao na amepanga kufanya video kali.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW