Burudani ya Michezo Live

Awalawiti watoto wawili kwa kuwaficha makaburini akiwatishia kuwaua kisha kuwapa tsh 500

Awalawiti watoto wawili kwa kuwaficha makaburini akiwatishia kuwaua kisha kuwapa tsh 500

Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara linamsaka mwanaume ambaye bado hajajulikana, aliyewalawiti watoto wawili wenye umri wa miaka Nane na mwingine miaka Tisa, baada ya kuwarubuni na kuwapa 500 na kisha kuwafanyia kitendo hicho, huku akiwatishia kuwaua kama hawatofuata atakacho waambia.

Akizungumza leo Januari 10, 2020, Kamanda wa Polisi mkoani humo Paul Kasabago, amesema kuwa mtuhumiwa huyo aliwachukua watoto hao, wakiwa njiani kuelekea shuleni majira ya saa 5:00 asubuhi.

“Mtuhumiwa huyo aliwalaghai kwa kuwapa Shilingi 500 ndiyo akawa amewavutia makaburini yaliyokaribu na shule hiyo na kuwalawiti kwa zamu, huku akiwatishia kwamba atawaua endapo hatokiri matakwa yake, watoto walitibiwa na kuruhusiwa na tunaendelea kumtafuta huyo mtuhuniwa” amesema Kamanda Kasabago.

Katika hatua nyingine Michael Donati (25), amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la ubakaji wa mwanafunzi wa Darasa la Sita.

Chanzo Eatv.tv

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW