Burudani

AY afungua kampuni

AYMsanii Ambwene Yessaya a.k.a mzee wa Commercial hivi karibuni ametangaza kufungua kampuni itakayokuwa ikijihusisha na masuala mbali mbali ya kisanii ikiwa ni kusimamia shughuli za aina tofauti za wasanii wa hapa nchini na nje ya nchi kwa ujumla.

AY

 

Msanii Ambwene Yessaya a.k.a mzee wa Commercial hivi karibuni ametangaza kufungua kampuni itakayokuwa ikijihusisha na masuala mbali mbali ya kisanii ikiwa ni kusimamia shughuli za aina tofauti za wasanii wa hapa nchini na nje ya nchi kwa ujumla.

 

 

 

Kampuni hiyo ambayo itajulikana kwa jina Unity Entertaiment Company Limited ambapo inatarajiwa kuanza kufanya shughuli zake rasmi mwanzoni mwa mwezi February ambapo mpaka sasa ni wasanii wasiozidi sabini wamethibitisha kujiunga na kampuni hiyo ikiwa ni wa ndani ya nchi na nje ya nchi.

 

 

 

“ Zaidi tumelenga kwa wasanii wa hapa nyumbani na nje ya nchi, kuna mapromota wengi wangependa kufanya kazi na wasanii tofauti, sasa unakuta mawasiliano hana, hivyo anakuja ofisi za Unity Entertainment.Co.ltd au anafanya mawasiliano na ofisi anaelezea msanii anayemuihitaji Tunampatia kwa makubaliano ya kiofisi zaidi na yule msanii pia naye tunamsimamia kwa kila kitu mpaka malipo yake yote analipwa na mambo yanaenda sawa, Pia kuwatafutia wasanii wetu shows za nje ya nchi kwa wasanii wa hapa nyumbani na wasanii wa nje nina mawasiliano ya karibu sana nao hivyo nawatafutia shows za hapa nchini na vilevile wandaaji wa matamasha wa hapa nchini wakiwa wanahitaji wasanii wa nje wanaweza kufanya mawasiliano na kampuni ya Unity hivyo inahakiki kuwa wanapata wasanii husika” alijielezea Ambwene.

 

 

 

Hii ni hatua ambayo ni dhahiri inastahili pongezi kwa msanii huyu kwa kuwa na wazo kama hili inaonesha ni namna gani shughuli za burudani hapa nchini zinaweza kufanyika katika mpangilio unaostahili na pia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana na dhana ya kuwa muziki ni uhuni.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents