AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

AY akubali walichofanya Fid Q, One, Wakazi, Songa na wengineo katika Bongo na Flava Film

Miongoni mwa movie zilizotoka Bongo mwezi huu, April na kuzungumzwa sana ni ile iitwayo Bongo na Flava Film ambayo wamecheza wasanii kama One The Incredible, Wakazi, Fid Q, Makamua, Songa, Saigon, Salu T na wengine.

Sasa msanii AY mara baada ya kuona movie hiyo amewaka wasanii wengine kufanya kitu kama hicho.

“Kabla movie yote hii hajaanza kuongelewa nilikaa nakaonyeshwa hiyo movie na nikazubaa muda wote kwa sababu mimi muda mwingi huwa nakaa na kucheza na masimu kuongea huku na kule lakini kiukweli nilipenda,” amesema AY.

“All best kuanzia hapa mmefungua njia, basi na wengine wafuate tu,” amesisitiza.

Soma Pia; Tazama filamu waliyocheza One The Incredible, Wakazi, Fid Q, Songa na wengineo

Wengine walioshiriki katika movie hiyo ni pamoja na Godliver, Karabani, Lamar, J Nkwabi, Silipa na Nkwabi.

Baadhi ya nyimbo zilizosikika katika filamu hiyo ni kama Juhudi za Wasiojiweza ya Fid Q aliyomshirikisha Bibi Kidude, Haya Maisha ya One The Incredible aliyomshirikisha Songa, Mara Hoo ya Bou Nako aliyomshirikisha JCB na Sugua Gaga ya Shaa.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW